pmbet

Nyota Arsenal apagawa na kinda Mtanzania

Sisti Herman

February 23, 2024
Share :

Kinda wa Tanzania, Harrith Chunga Misonge ambaye yupo Nchini Urusi anakoshiriki mashindano ya Games of the Future, amekutana na nyota wa zamani wa Arsenal na tỉmu ya taifa ya Urusi, Andre Arshavin ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mechi za mashindano hayo jijini Kazan.

 

Arshavin alionekana kuvutiwa na Harrith ambaye ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Aghakhan ya jijini Dar es Salaam na kuzungumza naye kwa dakika zisizopungua kumi.

 

“Aliniuliza nafasi ninayocheza lakini pia aliniuliza nchi ninayotoka akaniambia kwamba amewahi kufika Zanzibar na alivutiwa na fukwe zake alizozifananisha na fukwe za Maldives,” alisema Harrith.

 

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 12, amewekwa katika timu ya Franklins Bumblebee ambayo inajumuisha wachezaji watano kutoka katika mataifa mbalimbali duniani huku akionyesha kiwango cha kuvutia.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet