Nyota Cameroon wasimamishwa kisa kundanya Umri
Sisti Herman
March 11, 2024
Share :
Shirikisho la soka Cameroon limewasimamisha wachezaji 62 kwa kughushi umri akiwemo kiungo wa klabu ya Victoria United, Wilfried Nathan Douala (PICHANI) ambaye alichaguliwa katika kikosi cha Cameroon kilichoshiriki michuano ya AFCON 2023.
Wachezaji hao pamoja na Wilfried Douala anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 17 wamesimamishwa kwa kudanganya umri wao halisi. Douala alikuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kwenye AFCON 2023.