Nyota wa Real Madrid watemwa kwenye kikosi cha Kombe la Dunia 2026.
Joyce Shedrack
May 25, 2026
Share :
Kocha wa timu ya Taifa ya Uhispania Luis de la Fuente ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya Michuano ya Kombe la Dunia huku kwa mara ya kwanza katika historia la Taifa hilo akikosekana mchezaji hata mmoja wa Real Madrid aliyejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya mashindano makubwa.
Kikosi hicho kimejumuisha wachezaji 8 wa klabu ya Barcelona wakiwemo Lamine Yamal, Pedri, Gavi na Dani Olmo huku nyota wa Real Madrid kama Dean Huijsen, Raúl Asencio, Dani Carvajal, Ávaro Carreras, Fran García, Dani Ceballos na Gonzalo García wakiwa si sehemu ya wanajeshi hao wa Uhispania.

“Ni uamuzi mgumu,”Tumezingatia kila hali inayoweza kutokea kwenye mechi dhidi ya wapinzani wetu na tumechagua kikosi hiki. Sijali mchezaji anatoka klabu gani.”amesema De la Fuente alipoulizwa kuhusu uteuzi huo.
Mabingwa hao wa Ulaya mwaka 2024 wataanza kampeni zao za Kombe la Dunia la FIFA 2026 dhidi ya Cape Verde Juni 15 kabla ya kukutana na Saudi Arabia Juni 21 na kuhitimisha hatua ya makundi dhidi ya Uruguay Juni 27 wakiwa Kundi H.





