Nyota watano wa Liverpool kuikosa Man City.
Joyce Shedrack
February 6, 2026
Share :
Liverpool itawakosa hadi wachezaji watano watakapokabiliana na Manchester City katika Ligi Kuu nchini Uingereza Jumapili hii huko Anfield.
Meneja Arne Slot amesema wachezaji waliojeruhiwa huenda wasiwe fiti vya kutosha kucheza katika mechi kubwa.
Huenda mlinzi Joe Gomez yuko tayari kurudi, lakini bado hajaanza mazoezi baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Bournemouth karibu wiki mbili zilizopita.
Wachezaji wa majogoo hao wa London ambao bado wapo nje ya uwanja ni Jeremie Frimpong, Alexander Isak, Giovanni Leoni, na Conor Bradley.
Manchester City nao wanakabiliwa na changamoto za majeraha, huku Josko Gvardiol na John Stones wakiwa nje ya uwanja kutokana na majeraha, hii ilisababisha uhamisho wa hivi karibuni wa City kwa Marc Guehi, ingawa Ruben Dias amerejea mazoezini, na kutoa matumaini kidogo.





