Nyota wawili Fountain Gate wajiunga na Rayon Sports ya Rwanda
Sisti Herman
July 28, 2024
Share :
Wachezaji wawili waandamizi akiwemo Nahodha wa Fountain Gate Princess Aquila Gasper na Mshambuliaji Rehema Mohamed Ramadan, wamejiunga na Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda kwa mkataba wa mkopo wenye kipengele cha kuuzwa moja kwa moja kama wakikiwasha.
Wachezaji hao watacheza michezo ya kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika Kanda ya Afrika mashariki na kati (CECAFA).
Kwenye michuano hiyo Rayon Sports ambao ni wawakilishi wa Rwanda wpo kundi A na timu za CBE ya Ethiopia, Kenya Police ya Kenya, Yei Joints ya Sudan Kusini na Worriors Queens ya Zanzibar.
Pia wawilishi pekee wa Tanzania Simba Queens wapo kundi B wakiwa na timu za PVP Buyenzi ya Burundi, Kawempe Ladies ya Uganda na FAD Djibouti.