Nyumba ya mtoto wa Mbowe kupigwa mnada
Eric Buyanza
February 15, 2024
Share :
Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi imeamuru kukamatwa na kupigwa mnada kjwa nyumba ya mkurugenzi wa gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe iliyoko Mikocheni, ili kulipa deni la Shilingi milioni 62.7 anazodaiwa na waliokuwa waandishi na wahariri wa gazeti hilo baada ya mwajiri huyo kuvunja mikataba yao ya ajira.
Uamuzi huo wa mahakama umetolewa jana, Dar es Salaam, mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Mary Mrio baada ya kupitia hoja za washinda tuzo katika Tume la Usuluhishi na Uamuzi(CMA) Julai 2023.
Shauri hilo namba 28461 la mwaka 2023, wadai Maregesi Paul na wenzake tisa dhidi ya Mkurugenzi wa Gazeti la Tanzania Daima, Dudley Mbowe.