pmbet

Okello aaga rasmi na kuacha ujumbe mzito Jangwani

Eric Buyanza

August 21, 2026
Share :

Baada ya kutambulishwa na klabu Far Rabat ya nchini Morocco, kiungo mshambuliaji Allan Okello ameiaga rasmi Yanga kwa kuandika ujumbe.

 

Okello ambaye ni raia wa Uganda ameiaga timu hiyo na kumshukuru kila mtu aLiyefanya nae kazi ndani ya kikosi hicho cha Mtaa wa Twiga na Jangwani.

 

Okello ameandika “Asante Yanga kwa kuniamini na kwa kuufanya muda wangu mfupi katika klabu hii kubwa ya mpira wa miguu kuwa maalum kweli.

 

“ Ninashukuru kwa kila wakati, kila somo, msaada kutoka kwa Wanahabari, wachezaji wenzangu, makocha, wafanyakazi na muhimu zaidi ni mashabiki.

 

“ Naondoka kufuata changamoto nyingine. Naondoka nikiwa na moyo uliojaa shukrani na kumbukumbu zisizosahaulika, imekuwa heshima kuvaa jezi ya kijani na njano. Asante Yanga. Mna nafasi maalum maishani mwangu” aliandika Okello

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet