Okello kwenye rada za Fenerbahce
Sisti Herman
May 13, 2026
Share :

Wakala wa FIFA kutoka nchini 🇺🇬Uganda Ronnie Santos Mwine Fred ameripoti kuwa, Maskauti wa vigogo wa Uturuki Fenerbahçe SK wamekuwa Tanzania kwa siku ya 4 sasa wakimfuatilia nyota kijana wa timu ya taifa ya Uganda "The Cranes" Allan Okello.
Na Watamfuatilia tena katika mchezo ujao dhidi ya Dodoma Jiji.
Katika mechi ya kwanza waliyomtazama, alifunga mabao 2 na kutoa assist 1 dhidi ya Coastal Union
Young Africans S.C. wanatajwa kuhitaji takribani dola milioni 3 (Tsh 7.8B) kwa nyota huyo wa timu ya taifa ya Uganda, The Cranes.





