Okrah kufanyiwa vipimo zaidi
Sisti Herman
January 5, 2024
Share :
Winga mpya wa Yanga, Augustine Okrah mwenye umri wa miaka 30 jana kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Mapinduzi Cup dhidi ya KVZ ya Zanzibar alipata jeraha la kichwa dakika tatu baada ya kuingia uwanjani na kushindwa kuendelea na mchezo.
Taarifa kutoka Yanga zinaeleza kuwa Okrah anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya kitabibu zaidi kuhakikisha afya yake inakaa sawa kabla ya kuendelea na majukumu yake.