Okrah ni Mwananchi
Sisti Herman
January 1, 2024
Share :
Yanga jana usiku imemtangaza rasmi usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Augustine Okrah akitokea Bechem United ya Ghana.
Kabla ya kujiunga na Benchem Okrah alikuwa akiitumikia Simba katika msimu wa 2022/2023 na kutokufanya vizuri hadi kuondolewa kwenye kikosi hicho.
Akiwa na Bechem Okrah amekuwa akifanya vyema kwenye Ligi Kuu ya Ghana na hadi kuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba na katika mechi 16 ametupia mabao tisa.