Onana atua Al Hilal kutoka Simba
Sisti Herman
August 21, 2024
Share :
Klabu ya Al Hilal Benghazi ya Libya imetangaza kukamilisha uhamisho wa aliyekuwa winga wa klabu ya Simba Leandre Willy Essomba Onana (24) raia wa Cameroon.
Onana jana kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii aliwashukuru na kuwaaga mashabiki, wananchama na familia nzima ya klabu ya Simba kwa wakati waliokuwa pamoja.