"Onana ni Ronaldo Mtupu" - Ahmed Ally
Sisti Herman
March 10, 2024
Share :
Baada ya kufunga goli la ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union wakiibuka na ushindi wa 2-1, kiungo mshambuliaji wa Simba Esomba Onana amefananishwa na nyota wa Ureno na Al Nassr Cristiano Ronaldo.
Si mwingine aliyemfananisha na Ronaldo, bali ni yuleyule mwamba wa kauli tata kutoka unyamani Ahmed Ally, meneja wa idara ya habari na mawasiliano Simba ambaye siku za nyuma aliuaminisha uma kuwa mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Cameroon Samuel Etoo kuwa “Onana ni mali”
Jana baada ya mchezo msemaji huyo alichapisha picha ya Onana na kuandika “Ronaldo Mtupu”
Je maneno ya Ahmed Ally yana uhalisia kiasi gani?