Opah Clement aanza kukiwasha rasmi ligi kuu China
Sisti Herman
July 29, 2024
Share :
Nahodha wa timu ya Taifa Wanawake Tanzania Opah Clement amejiunga na kuanza kuitumikia rasmi klabu yake mpya ya Henan Jianye FC ya ligi kuu wanawake nchini China akitokea klabu ya Besitkas ya ligi kuu Uturuki.
Opah siku moja tu baada ya kutambulishwa alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu nchini humo huku timu yake ikipoteza 1-0 nyumbani.
Ligi ya China ipo mzunguko wa 13 huku timu ya Opah ikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi hiyo.
Kila la kheri Captain @opah_clement