Orlando Pirates inategemea sana Uchawi - Teko Modise
Sisti Herman
April 6, 2025
Share :
Baada ya wiki hii kocha mkuu wa klabu ya Orlando Pirates Jose Riveiro kutangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, aliyekuwa nguli wa zamani wa timu ya Taifa ya Afrika kusini na klabu za Orlando Pirates na Mamelodi Sundowns Teko Modise anaamini moja kati ya sababu za kocha huyo kutaka kuondoka Pirates ni klabu hiyo kutegemea zaidi masuala ya ushirikina.
“Nimecheza timu tofauti lakini sijawahi kuona timu inayotumia Muti (uchawi ) kama Orlando pirates"
"Walitaka niende kuoga na Muti kwenye bwawa kwa muda wa saa 2 asubuhi nikakataa"
"Nadhani hii ndio maana Jose Riveiro ataondoka"
Modise baada ya Riveiro kutangaza kuondoka, maneno hayo pia ameyaandika kwenye kitabu cha maisha yake ya soka akiwa na Orlado Pirates.