Orlando Pirates wamtaka Aziz Ki kwa hali na Mali
Sisti Herman
April 9, 2024
Share :
Jarida la KickOff la nchini Afrika kusini limethibitisha kuwa klabu ya Orlando Pirates imeulizia uwezekano wa kumpata kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Stephanie Aziz Ki ambaye mkataba wake na klabu hiyo unafikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu.
Orlando wanaongoza mbio za kuipata saini ya Ki huku wapinzani wao wakubwa Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns wakionyesha nia kubwa ya kuhitaji saini ya mchezaji huyo kutokea nchini Burkinafaso.