Oscar atoka hospital
Sisti Herman
November 17, 2025
Share :

Kiungo wa zamani wa Chelsea na Brazil Oscar ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kulazwa wiki iliyopita kutokana na tatizo la moyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 aliugua alipokuwa akifanyiwa majaribio ya kimwili kabla ya msimu mpya katika kituo cha mazoezi cha Sao Paulo cha Brazil Jumanne.
Sao Paulo aimema katika taarifa yake Oscar aliondoka Hospitali ya Einstein Israelta siku ya Jumapili na alikuwa "imara na yuko vizuri kiafya" katika muda wote wa kukaa kwake.





