Osimhen amwaga machozi mashabiki wakimuenzi marehemu mama yake.
Joyce Shedrack
March 11, 2026
Share :
Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen usiku wa jana alimwaga machozi akiwa uwanjani wakati mashabiki wa Galatasaray walipomuenzi mama yake ambaye ni marehemu kwa tifo kubwa kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool FC.
Dakika chache kabla ya mchezo kuanza katika uwanja wenye shamrashamra wa Rams Park, mashabiki wa nyumbani waliinua tifo kubwa yenye kugusa moyo, iliyokuwa na picha ya mshambuliaji huyo wa Nigeria pamoja na mama yake a,baye ni marehemu.

Bango hilo lilikuwa na ujumbe wenye nguvu uliomgusa sana mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 uliandikwa maneno yafuatayo:
“Sisi ni familia, na familia ni kila kitu.”
Wakati wimbo wa Champions League ulipokuwa ukisikika, Osimhen alionekana akilia akiwa amesimama kwenye mstari pamoja na wachezaji wenzake Mario Lemina na Gabriel Sara. Kiungo Lucas Torreira alionekana akimfariji mshambuliaji huyo kabla hajitulia na kuanza kusalimiana na wachezaji wa Liverpool.
Licha ya hisia hizo, za kumpoteza mama yake mzazi hivi karibuni lakini Osimhen aliendelea kuonesha ubora wake akiwa uwanjani baada ya kutoa pasi ya bao kwa Mario Lemina aliyefunga bao pekee katika ushindi muhimu wa 1–0 kwa Galatasaray.





