pmbet

Osimhen na mpenzi wake Stefanie wakaribisha mtoto wao wa pili

Eric Buyanza

October 30, 2026
Share :

Mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki, Victor Osimhen, na mpenzi wake wa muda mrefu, Stefanie Kim Ladewig, wamepata mtoto wao wa pili (wa kike).

 

Klabu ya Galatasaray ilithibitisha habari hizo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, ikimpongeza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na mpenzi wake kwa kumpata mwanachama mpya katika familia yao. Mtoto huyo amepewa jina la Liora Audrey.

 

"Mchezaji wa Timu yetu ya Wanaume, Victor Osimhen na Stefanie wameejaliwa kupata mtoto wa kike. Tunawapongeza sana Victor na Stefanie, na tunamwombea mtoto wao mchanga, Liora Audrey, maisha marefu, yenye afya na furaha!" ilieleza taarifa ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uturuki (Süper Lig).

Malaika huyo mpya anaungana na mtoto wao wa kwanza wa kike, Hailey True, ambaye alizaliwa mwezi Oktoba mwaka 2022.

 

Osimhen na Stefanie, ambaye ni mwanamitindo mwenye asili ya Ujerumani na Cameroon, walianza mahusiano yao tangu mwaka 2019 wakati mchezaji huyo alipokuwa akikipiga katika klabu ya Wolfsburg nchini Ujerumani.

 

Kuzaliwa kwa mtoto Liora Audrey kunakuja wiki chache tu baada ya Stefanie kuripotiwa kupata ajali ndogo ya gari jijini Istanbul akiwa mjamzito, lakini alitoka salama bila majeraha yoyote.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet