Otto Addo aishtaki GFA FIFA kisa kusitishiwa mkataba
Sisti Herman
October 31, 2026
Share :

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana 'Black Stars', Otto Addo, amelishtaki shiriki-sho la soka la nchi hiyo ‘GFA’ katika Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Addo amechukua hatua hiyo ya kisheria kufuatia uamuzi wa GFA kusitisha mkataba wake ghafla mapema mwaka huu, hatua iliyokuja baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo ya timu hiyo wakati ikijiandaa na Kombe la Dunia 2026.
Kocha huyo ameitaka FIFA kumsaidia kupata stahiki zake, ikiwemo fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wake uliokuwa umebakiwa na miezi 10 na malimbikizo ya mishahara.
Sakata hilo linatarajiwa kuchukua sura mpya na kuiongezea presha GFA, ambayo imekuwa iki-laumiwa kwa uamuzi wa haraka wa kufukuza makocha bila kufuata taratibu za kimkataba.
Addo, ambaye alikuwa akipokea mshahara wa dola 50,000 (takribani Sh135 milioni) kwa mwe-zi kabla ya kufukuzwa Machi 31, ameeleza kusikitishwa na namna alivyoondolewa bila sababu za msingi.





