pmbet

Ozil kuishabikia Spurs leo kisa Arsenal

Sisti Herman

May 14, 2024
Share :

Wakati mashabiki wengi wa Arsenal Ulimwenguni kote leo 'wakijitoa ufahamu' kwa kuungana na mahasimu wao wa jadi Tottenham Hotspur katikati kushinikiza Spurs kuifunga Manchester City ili kurahisisha Ubingwa kwenda upande wao, kiungo wa zamani wa Arsenal Mesut Ozil amechapisha ujumbe wa kushabikia Spurs ili waifunge City leo.

"Kwa mara ya kwanza leo usiku (nitawashabikia), Twendeni Spurs, msipoteze mchezo sitawatania tena, nawaahidi" aliandika Ozil kupitia mtandao wake wa 'X'.

Ozil ambaye alicheza Arsenal ameendelea kuwa shabiki wa klabu hiyo kama wachezaji wengi waliocheza kwenye klabu hiyo.

Endapo Spurs wataifunga City leo, Arsenal wataendelea kuwa juu kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo imebakiza mchezo mmoja pekee kumalizika, lakini endapo City watashinda leo basi watapaa hadi juu kwenye msimamo wa ligi hiyo na kuwa na asilimia kubwa ya kutwaa taji hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet