P Diddy achunguzwa kuhusika na mauaji ya Tupac Shakur.
Joyce Shedrack
July 30, 2024
Share :
Mwanamuziki maarufu wa Hip-hop kutoka Marekani P Diddy ameripotiwa kufanyiwa uchunguzi na familia ya Marehemu Tupac Shakur aliyefariki Septemba 7,1996 baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye gari huko Las Vegas huku kesi ya mauaji yake ikiendelea kulindima Mahakamani kwa zaidi ya miaka 20.
Taarifa mbalimbali kutoka nchini humo zinaeleza kuwa familia ya marehemu Tupac imeajiri wanasheria nguli akiwemo Alex Spiro na Christopher Clore kufuatilia madai ya Diddy kuhusika na kifo cha Tupac huku wakiamini huwenda mwanamuziki huyo anafahamu kitu kuhusu tukio la mauaji ya ndugu yao.
Diddy anaripotiwa kumlipa dola milioni 1 sawa na Sh 2 bilioni mtuhumiwa namba moja ambaye kwa sasa yupo gerezani Keef D kukamilisha tukio hilo.
Taarifa za madai hayo dhidi ya Diddy zimeibuka baada ya wiki iliyopita wakati Keefe D akiwa mahakamani kudai yeye na wafanyakazi wenzake walilipwa fedha kukamilisha mauaji ya Tupac katika miaka ya 90s.