pmbet

P Diddy apiga bei mjengo wake kwa Bilioni 185.8.

Joyce Shedrack

July 4, 2024
Share :

Nyota wa Hip-hop kutoka Marekani Diddy Combs ameuza nyumba yake ya kifahari iliyofanyiwa upekuzi na Polisi mapema mwezi wa tatu mwaka huu Jijini Los Angles Marekani kwa dola milioni 70 ikiwa ni sawa na Sh 185.8 bilioni.

 

Diddy amefanya uamuzi huo ikiwa ni miezi mitatu imepita tangu machi 25, 2024 siku ambayo  nyumba zake mbili ikiwemo ya Los Angeles na Miami kufanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa ikiwa ni uchunguzi wa kesi ya biashara ya ngono inayomkabili msanii huyo. 

Taarifa zinasema sababu kubwa ya Diddy kufanya uamuzi wa kuuza nyumba yake hiyo ni ili kuhama kabisa jijini Los Angeles.

Tangu mwaka jana mwishoni rapa huyo amekuwa akiandamwa na kesi nyingi za biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia lakini licha ya kufunguliwa kesi zaidi ya 6 bado haujapatikana ushahidi mkubwa wa kumtia nguvuni mwanamuziki huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet