pmbet

P DIDDY Apotgeza ushahidi afuta picha zote instagram.

Joyce Shedrack

June 21, 2024
Share :

Rapa kutoka Marekani Sean Combs maarufu P Diddy amepitisha fagio kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kufuta machapisho yote aliyowahi kuchapisha ikiwemo video yake ya kuomba radhi kufuatia video iliyowahi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ya tukio la kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie Ventura  lililotokea hotelini mwaka 2016.

Rapa huyo alifuta picha pamoja na video zote siku ya jana Alhamis Juni 20 jambo lilopelekea akaunti yake  kuanza kupoteza wafuasi waliokuwa wanamfatilia kupitia mtandao huo. 
 

Tangu mwaka jana Diddy amekuwa akiandamwa na kesi zinazomuhusisha na biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia kesi ambazo zimekuwa zikikosa ushahidi wa nguvu wa kusababisha kusalia mikononi mwa polisi.

 

Baadhi ya wasanii  wamekuwa wakimuhisi rapa huyo kuwa miongoni mwa jeshi la FBI akiwemo mmiliki wa Death Row Records Suge Knight ambaye aliwahi kumtaja msanii huyo kama miongoni mwa watu wa kuogopwa. 
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet