Pacome aachwa kikosi cha Afcon
Sisti Herman
December 29, 2023
Share :
Baada ya kujumuishwa kwenye kikosi cha awali na kocha wa timu ya Taifa ya Ivory Coast Mfaransa, Jean-Louis Gasset, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoa ameachwa baada ya mchujo wa kupata kikosi cha mwisho kuwakilisha Taifa hilo ambapo wamepenya wachezaji 27 kwa ajili ya michuano ya kombe la Mataifa Afrika AFCON 2023 itakayoanza kurindima kuanzia ya Januari 13, 2024.
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Sebastien Haller, beki wa Monaco Wilfried Singo na viungo Ibrahim Sangare wa Nottingham Forest ya Premier League, Seko Fofana (Al Nassr) na Franck Kesslie (Al Ahli) ni miongoni mwa nyota walioitwa huku mshambuliaji wa Galatasary Wilfried Zaha na beki wa Beskitas Eric Bailly walitemwa.
KIKOSI KAMILI
Magolikipa: Yahia Fofana (Angers/FRA), Charles Folly (Asec Mimosas), Badra Ali (Sekhukhune United/RSA).
Walinzi:
Serge Aurier (Nottingham Forest/ENG), Willy Boly (Nottingham Forest/ENG), Ismael Diallo (Hajduk Split,/CRO), Ousmane Diomandé (Sporting Lisbon/POR), Ghislain Konan (Al-Feiha/KSA), Evans N’dicka (Roma/ITA), Odilon Kossonou (Bayer Leverkusen/GER) Wilfried Singo (Monaco/FRA)
Viungo: Jean-Thierry Amani Lazare (Union Saint-Gilloise/BEL), Idrissa Doumbia (Alanyaspor/TUR), Seko Fofana (Al Nassr/KSA), Ibrahim Sangaré (Nottingham Forest/ENG), Franck Kessié (Al-Ahli/KSA), Jean-Michael Seri (Hull/ENG).
Washambuliaji: Simon Adingra (Brighton/ENG), Jonathan Bamba (Celta Vigo/ESP), Jérémie Boga (Nice/FRA), Sébastien Haller (Borussia Dortmund/GER), Karim Konaté (RB Salzburg/AUT), Christian Kouamé (Fiorentina/ITA), Jean-Philippe Krasso (Red Star Belgrade/SRB), Max-Alain Gradel (Gaziantep/TUR), Oumar Diakité (Reims/FRA), Nicolas Pépé (Trabzonspor/TUR).
Ivory Coast imepangwa Kundi A pamoja na Guinea-Bissau, Nigeria na Equitorial Guinea.