Pacome aitwa Ivory Coast
Sisti Herman
March 19, 2024
Share :
Baada ya kuwakosa viungo wake washambuliaji Seko Fofana na Ibrahim Sangare kwenye kipindi hichi cha michezo ya kimataifa Kocha wa timu ya Taifa ya Ivory Coast Emerse Fae amemuita Kiungo wa Klabu ya Yanga Sc Pacome ZouZou, kuchukua nafasi ya Ibrahim Sangare, anayeitumikia Klabu ya Nottingham Forest ya Uingereza baada ya mchezaji huyo kupata majeraha.
Ikumbukwe kuwa Pacome ZouZou, hakumaliza mchezo wa DarDerby baina ya Azam Fc dhidi ya Yanga Sc baada ya mchezaji huyo kupata majeraha na kulazimika kutolewa nje kwa lazima.
Sasa itakuwaje…?