Pacome Day ni kupaka Bleach tu
Sisti Herman
February 19, 2024
Share :
Klabu ya Yanga imetangaza kuwa mechi yao ya kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad itakuwa siku ya kiungo Pacome Zouzoua PacomeDay.
Meneja wa idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ali kamwe amesema kwa pamoja uongozi na wachezaji wamekubaliana kuifanya mechi hiyo kuwa maalum kwa Pacôme Zouzoua.
Ali Kamwe amebainisha kuwa mtoko wa siku hiyo ni mwendo ‘bleach’ iwe kichwani ama kwenye kidevu.