Pacome Zouzoua ndo basi tena hatacheza Yanga msimu ujao.
Joyce Shedrack
July 28, 2026
Share :
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe amethibitisha kuwa mchezaji wao raia wa Ivory Coast Pacome Zouzoua atakosekana msimu mzima kwenye kikosi chao kutokana na majeraha aliyoyapata.
Ally Kamwe ameweka wazi kuwa Pacome hatakuwa sehemu ya kikosi chao lakini atapatahaki zake zote kimkataba huku akiendelea kuuguza jeraha lake.
Ikumbukwe kuwa Pacome alipata jeraha baya la kuvunjika mguu wake kwenye mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya JKT Tanzania kwenye uwanja wa Meja Isamuhyo na kusababisha kufanyiwa upasuaji wa mguu.





