Padri mbaroni kwa Utapeli
Sisti Herman
February 13, 2024
Share :
Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bunda mkoani Mara, Karoli Mganga akishirikiana na Mhasibu wa Parokia hiyo, Gerald Mgendagenda wanashiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia zaidi ya shilingi milioni 800 kinyume cha sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salim Morcase amesema kutokana na tuhuma hizo, jeshi hilo liliwakamata watuhumiwa wote wa wawili kwaajili ya uchunguzi. Kamanda amesema Paroko huyo na Mhasibu wake wanadaiwa kughushi nyaraka kwa nyakati tofauti na kujipatia fedha hizo ambazo ni mali ya parokia hiyo ambapo ni kinyume cha sheria na taratibu.
Amesema mbali na kughushi nyaraka hizo, pia watuhumiwa hao wanadaiwa kughushi sahihi za watu mbalimbali zilizowawezesha kufanikisha malengo yao.