pmbet

'Pair' ya ndugu watano watakaocheza kombe la Dunia 2026.

Joyce Shedrack

June 5, 2026
Share :

Kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026, kuna jumla ya pea 5 ya wachezaji ambao ni ndugu wa damu wanaoshiriki michuano hii kwa wakati mmoja, ambapo baadhi yao wanachezea timu moja na wengine mataifa tofauti.

Ndugu Wanaochezea Taifa Moja ni Jurriën na Quinten Timber (Uholanzi): Mapacha wenye kipaji kikubwa wamefanikiwa kuingia pamoja kwenye kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Uholanzi.

  •  

    Lucas na Theo Hernández (Ufaransa): Mabeki wa kushoto wenye asili ya Uhispania wanalitetea tena taifa la Ufaransa kwa pamoja. 

  •  
  • Leandro na Juninho Bacuna (Curaçao): Ndugu hawa wanaiongoza nchi yao ndogo ya Curacao iliyoweka historia ya kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa. 

 

Ndugu Wanaochezea Mataifa Tofauti

  • Guéla Doué na Désiré Doué: Kaka mkubwa,Gela Doue anaichezea timu ya taifa ya Ivory Coast, wakati mdogo wake, Désiré Doué, amechaguliwa kuichezea Ufaransa.
  •  
  • Iñaki Williams na Nico Williams: Iñaki anaichezea timu ya taifa ya Ghana, wakati mdogo wake Nico anawakilisha Uhispania. 
pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet