Palace wanataka pauni milioni 60 ili kumuachia Olise kwa Man United
Eric Buyanza
April 26, 2024
Share :
Klabu ya Manchester United italazimika kulipa pauni milioni 60 ili kumpata Michael Olise kutoka Crystal Palace.
Olise amefunga mabao 7 na assist 4 katika mechi 15 pekee na hilo limeonekana kuwavutia Man Utd.
Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akivutiwa kwa muda mrefu na United, ambao wanataka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji msimu ujao.