pmbet

Palmer amtishia Halland, afunga Hat-trick

Sisti Herman

April 16, 2024
Share :

Mara baada ya jana kufunga magoli manne kati ya 6-0 waliyoshinda dhidi ya Everton kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza, Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Cole Palmer sasa amefikisha jumla ya magoli 20 kwenye ligi kuu Uingereza msimu huu akifungana idadi na mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Erling Halland.

Licha ya Palmer kumfikia Halland kwa idadi ya magoli lakini pia amemzidi mshambuliaji huyo kwa kuchangia idadi kubwa ya magoli kwani Palmer amefikisha pasi za mabao 9 hadi sasa huku Halland akiwa nazo 5 hadi sasa.

 

Palmer ni mchezaji wa kwanza wa Chelsea kufunga mabao manne kwenye mchezo mmoja tangu Frank Lampard alivyofanya hivyo dhidi ya Aston Villa mwaka 2010.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet