Palmer; Wachambuzi wapo sahihi kukosoa lakini kocha ndo mwenye maamuzi ya mwisho
Sisti Herman
June 26, 2024
Share :
Baada ya kushuhudia ukosoaji mkubwa kutoka kwa wadau wa soka nchini Uingereza hasa wachezaji wa zamani ambao ni wachambuzi kwenye televisheni kubwa kuhusu mambo mbalimbali kwenye timu ya taifa ya Uingereza inayoshiriki michuano ya kombe la Mataifa Ulaya (Euro 2024) kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Cole Palmer amesema kuwa ushauri na ukosoaji wao ni mzuri lakini kocha ndo mwenye maamuzi ya mwisho.
"Ni ushauri mzuri hasa kwa mtu kama Roy Keane aliyefanikiwa kimataifa na hata akiwa na Man Utd lakini kuna muda mwalimu ndo anajua anachohitaji" alisema Palmer baada ya mchezo wa jana dhidi ya Slovenia.
Wachambuzi hao wamekuwa wakikosoa mbinu za k0ocha huyo hasa upangaji wake wa kikosi, wengi wakikosoa kuachwa nje kwa nyota kama Cole Palmer na Kobe Mainoo ambao kila wakipata nafasi huwa na matokeo chanya uwanjani.
Uingereza ilipata sare ya pili jana kwenye michuano hiyo huku hadi sasa ikicheza michezo mitatu na kufunga mabao mawili pekee yaliyowawezesha kufuzu hatua ya mtoano wakiwa juu kwenye msimamo wa kundi.