pmbet

Pambano kubwa la ngumi kuchezwa kwa mara ya kwanza Misri

Eric Buyanza

February 28, 2026
Share :

Mabondia Oleksandr Usyk na Rico Verhoeven watazichapa Mei 23, 2026, kwenye mapiramidi ya Giza nchini Misri, ambapo Oleksandr atakuwa akitetea mkanda wake wa WBC. 

Usyk, ambaye hajawahi kushindwa kwenye mapambano ya kulipwa, atakuwa akimkabili Verhoeven ambaye ni mpiganaji wa zamani wa kickboxing aliyeshinda ubingwa wa dunia mara moja. 

Pambano hilo, linaloitwa "Glory in Giza," litatangazwa moja kwa moja kwenye DAZN, na ni pambano la kwanza la ubingwa wa dunia la uzito wa juu kutokea nchini Misri.

"Ninawaheshimu sana watu wanaofikia kilele katika mchezo wao," Usyk alisema Ijumaa. "Rico ni mmoja wao. Ninaheshimu safari yake....yeye ndiye mfalme wa kickboxing lakini huu ni mchezo wa ndondi, mchezo tofauti wenye sheria na wafalme wake." Alisema Usyk.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet