Pambano la Mwakinyo na mghana lafutwa
Eric Buyanza
May 28, 2024
Share :
Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), limefuta pambano la ngumi baina ya Hassan Mwakinyo dhidi ya bondia kutoka nchini Ghana, Pactick Allotey.
Sababu za kufutwa kwa pambano hilo zimeelezwa kuwa ni kutokana na promota pambano hilo kushindwa kukidhi vigezo.
Baadhi ya vigezo hivyo ni malipo ya mabondia, na pili ni ukumbi ambao lingechezwa pambano hilo kutofikia viwango vianavyostahili.