pmbet

Pamoja na kushinda, Kompany asema Madrid itabaki kuwa Madrid

Eric Buyanza

April 16, 2026
Share :

Kocha wa Bayern Munich, Vincent Kompany, amewasifu wachezaji wake kwa kupambana vyema na changamoto za kimchezo wakati walipokabiliana na Real Madrid katika mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
 

Mabingwa hao wa Bundesliga walihitaji mabao mawili ya dakika za lala salama kutoka kwa Luis Diaz na Michael Olise ili kuwashinda Madrid 4-3 kwenye Uwanja wa Allianz Arena Jumatano usiku.
 

"Ulikuwa mchezo wa hisia sana. Tulipata nafasi nyingi na kila mara tulihisi tunaweza kufunga. Lakini Real Madrid inabaki kuwa Real Madrid," Kompany aliwaambia wanahabari.
 

"Wana wachezaji wepesi sana na mara zote ni tishio.

"Vijana wangu walikuwa vyema kiakili leo, na mashabiki pia walitusaidia. Tulitulia na kila mara tulihisi kwamba wakati wetu ungefika. Vijana walistahili ushindi huu" alimalizia Kompany.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet