Pamoja na kuwindwa Uingereza, Barcelona wana imani dogo atasaini mkataba mpya
Eric Buyanza
April 15, 2024
Share :
Klabu ya Barcelona ina imani chipukizi wake Pau Cubarsi atasaini mkataba mpya licha ya vilabu vingi vya Premier League kuonesha nia ya dhati ya kumtaka.
Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 17 aliingia katika kikosi cha kwanza cha Barca mwanzoni mwa mwaka huu na ameimudu vyema nafasi yake. Cubarsi ameanzishwa kwenye kikosi cha kwanza mara 13 na amefanikiwa kucheza kwa dakika 90 hivi majuzi kwenye robo fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Paris Saint-Germain.
Kiwango kizuri cha Cubarsi umevivutia vilabu kadhaa vikubwa vya Ulaya, huku Chelsea na Manchester United wakihusishwa kutaka kumnunua.