pmbet

Panya Magawa ajengewa sanamu Cambodia

Sisti Herman

April 10, 2026
Share :

 

Cambodia imezindua sanamu maalum ya Panya Magawa kutoka Tanzania, Panya anayetajwa kuwa Shujaa aliyesaidia kugundua mabomu ya ardhini na kuokoa maisha ya Watu wengi katika Nchi hiyo ambayo imepanga kumaliza kabisa kuyaondoa mabomu yaliyotegwa ardhini ifikapo mwaka 2030.

Sanamu hii iliyochongwa kwa mawe ya eneo husika, imewekwa katika Mji wa Siem Reap na kuonyeshwa rasmi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa wa Migodi ambapo Magawa ameoneshwa akiwa amevaa kifaa chake cha kazi pamoja na medali aliyotunukiwa kwa ushujaa.

Panya Magawa alianza kazi Nchini Cambodia mwaka 2016 baada ya kufundishwa na Shirika la Apopo na kugundua zaidi ya mabomu 100 na vilipuzi vingine na akaweza kusaidia kusafisha zaidi ya mita za mraba 141,000 za ardhi sawa na viwanja takribani 20 vya mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano.

Kutokana na mchango wake huo, mwaka 2020 alitunukiwa Medali ya Dhahabu PDSA na kuwa panya wa kwanza kuipata katika historia ya Tuzo hizo ambapo baada ya kustaafu kutokana na uzee, Magawa alikufa mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka minane lakini kazi yake imeacha alama kubwa hasa ikizingatiwa kuwa Cambodia bado ni miongoni mwa Nchi zilizoathirika zaidi na mabomu ya ardhini yaliyosalia tangu vita za zamani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet