Papa Leo XIV aomba msamaha wa Kihistoria Vatican
Sisti Herman
May 27, 2026
Share :

Papa Pope Leo XIV ameomba rasmi msamaha kwa niaba ya Kanisa Katoliki kutokana na nafasi iliyochezwa na Holy See katika kuruhusu na kushindwa kupinga biashara ya utumwa kwa muda mrefu katika historia.
Katika waraka wake mpya, Papa huyo amesema historia hiyo imeacha “jeraha kubwa” ndani ya kumbukumbu ya Ukristo, huku akikiri kuwa taasisi za kanisa katika nyakati za zamani pia zilimiliki watumwa.
Amesema Kanisa lilichelewa kutoa msimamo wa wazi dhidi ya utumwa hadi karne ya 19 chini ya Papa Leo XIII, baada ya miaka mingi ya ukimya na mkanganyiko kuhusu suala hilo.
Kauli hiyo imeelezwa kuwa moja ya matamko makubwa zaidi kuwahi kutolewa na Papa kuhusu kuhusika kwa Vatican katika historia ya utumwa wakati wa ukoloni.





