Paramount yaiweka sokoni BET, wanaiuza kwa Trilioni 4
Sisti Herman
July 3, 2024
Share :
Kampuni ya burudani Paramount inayohusika na uzalishaji, utengenezaji, usimamizi na usambazaji wa maudhui kama Filamu na miziki pamoja na uandaaji wa tuzo za filamu na muziki ambapo pia inamiliki kampuni ya BET inayoandaa tuzo za BET, imeripotiwa kuwa kwenye mazungumzo ya kuiuza kampuni ya ‘BET’ kwa kiasi cha kati ya Tsh Trilioni 4.2/= - 4.5/= kwa wanunuaji akiwemo CEO Wa BET ‘Scott Mills Na Chinh Chu’.
Kwa mujibu wa jarida la Variety Mwaka jana 2023 Mwigizaji na Muongozaji wa filamu chini Marekani Tyler Perry aliripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na kampuni ya Paramount Global kwa ajili ya kununua hisa nyingi (majority stake) za kampuni ya BET ambapo ndani yake kuna vituo kama BET, VH1 na huduma za BET+ .
Wengine waliotaka kuinunua kampuni hiyo ni rapa na Mfanyabiashara 50 Cent, Diddy Pamoja Na Mabilionea Wengine.