'Paredi' la Yanga laanza na Supu kwa Mkapa
Sisti Herman
May 26, 2024
Share :
Kabla ya maandamano makubwa ya Ubingwa wao wa 30 wa ligi kuu Tanzania bara waliokabidhiwa jana 'Paredi la ubingwa' mashabiki wa klabu ya Yanga leo wameifungua siku na supu iliyoandaliwa na uongozi wa klabu hiyo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Paredi la Yanga litaanza Uwanja wa Taifa Temeke, Keko, Tazara, Bugeuruni, Ilala, Kariakoo kuelekea Makao makuu ya klabu hiyo kwa mujibu wa Ali Kamwe, afisa habari wa klabu hiyo.