Patino hana mpango wa kubaki Arsenal, vigogo ulaya wamfukuzia
Eric Buyanza
April 27, 2024
Share :
Kiungo wa kati wa Arsenal Charlie Patino huenda akaihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Ripoti zinasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 hana nia ya kusalia katika klabu hiyo ya Kaskazini mwa London.
Mchezaji huyo kwa sasa yuko kwa mkopo Swansea City na anafanya vyema akiwa amefunga mabao manne na kutoa assist 4 za mabao.
Vilabu kama Juventus na Roma vimeonesha nia ya kumsajili mwishoni mwa msimu huu na inaelezwa kuwa mwenyewe ana matamanio makubwa ya kucheza Italia.