Patrice Motsepe achaguliwa kuwa Rais wa CAF kwa miaka minne ijayo.
Joyce Shedrack
March 12, 2025
Share :
Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika Patrice Motsepe amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika kwa miaka minne ijayo hadi mwaka 2029.

Motsepe amechaguliwa kuongoza shirikisho hilo ikiwa ni mara ya pili mfululizo katika uchaguzi uliofanyika wakati wa mkutano mkuu wa CAF unaoendelea mjini Cairo, Misri.