pmbet

Patrick amruhusu swahiba wake ampachike mimba mkewe

Eric Buyanza

April 8, 2024
Share :

Kwa hali ya kawaida watu wana mipaka juu ya kile wanachosaidiana kama marafiki katika maisha, lakini jamaa mmoja huko nchini Kenya aliyefahamika kwa jina la Patrick amefanya jambo ambalo sio rahisi kwa wanaume wengi kulifanya. 

TUKO AMEFANYAJE? 

Patrick amemruhusu mshkaji wake kipenzi atembee na mke wake ili amtie mimba. ILIKUAJE? Patrick na mke wake mrembo Zubeda, walijaribu kwa miaka mingi kutafuta mtoto bila mafanikio hali iliyowalazimu kutafuta ushauri wa kitabibu ili kufahamu tatizo. "Baada ya kufanyiwa vipimo mimi niligundulika kuwa sina uwezo wa kumzalisha mke wangu." 

"Lakini hata hivyo sikukubaliana na hali hiyo nikaamua kutembea na wanawake wengine nje ya ndoa ili nijaribu kuona kama ningeweza kuwapa mimba lakini haikuwezekana. Ndipo nilipoamua kuomba msaada kwa rafiki yangu mkubwa," anasema Patrick. 

Rafiki wa Patrick alipopata habari hizo kwa mara ya kwanza alishtuka na kushangazwa na uamuzi wa Patrick wa kutaka alale na mke wake. 

KWA UPANDE WA ZUBEDA ILIKUAJE? 

Zubeda alichukia sana na hakukubaliana na wazo hilo, lakini aliingiwa na huruma alipoona mumewe hana furaha, ikambidi akubali kwa unyonge. Rafiki wa Patrick anasema...

“Patrick aliniomba jambo gumu sana, mwanzo nilisita lakini baadae baada ya kuwaza sana nilikubali kusaidia, nilizaa na mke wake watoto watatu, lakini tulikubaliana watakuwa wake. 

"Hao watoto siwaoni kuwa ni wangu kwasababu tulifanya makubaliano kisheria kwa ajili ya hilo, nina furaha nilimsaidia rafiki yangu, na sasa na yeye ni baba," alisema jamaa. 

Patrick anajigamba kuwa ndoa yake iko imara licha ya maamuzi magumu aliyochukua ili tu aweze kupata watoto.

TUKO

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet