Paul Scholes amvulia kofia Kobe Mainoo
Sisti Herman
May 26, 2024
Share :
Baada ya jana klabu ya Manchester United kutwaa ubingwa wa kombe la FA mbele ya watani zao Manchester City kwenye dimba la Wembley, Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amewaasa mashabiki wa klabu hiyo acha kumlinganisha na kiungo mshambuliaji kinda Kobe Mainoo ambaye jana alifunga goli moja kati ya mawili ya ushindi.
"Nimesoma maeneo tofauti nikilinganishwa na huyo kijana wiki iliyopita, jamani msipoteze muda wenu , amenizidi mara 10 zaidi" aliandika Scholes kuhusu kinda huyo.
Manchester imebeba ubingwa huo kwa ushindi wa 2-1 huku magoli yao yakifungwa na wachezaji kutoka kwenye Academy yao ya Carrington, Alejandro Garnacho na Kobe Mainoo ambao wamekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.
Goli la kufutia machozi la City limefungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Ubelgiji Jeremy Doku.