Pawasa aungana na Julio kuinusuru Singida kushuka daraja
Sisti Herman
April 5, 2024
Share :
Aliyekuwa beki na nahodha wa klabu ya Simba ambaye kwasasa ni kocha wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, Boniphace Pawasa yupo mbioni kujiunga na klabu ya Singida Black Stars kama kocha msaidizi ili kuinusuru klabu hiyo ambayo imekuwa na matokeo mabaya msimu huu kwenye hatari ya kushuka daraja.
Pawasa ambaye ameanza safari kuelekea jijini Mwanza anaenda kuungana na kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye alirithi mikoba ya kpcha Thabo Senong aliyeachana na timu hiyo wiki kadhaa zilizopita kutokana na matokeo yasiyoridhisha ambapo hadi sasa wapo nafasi 11 kati ya timu 16 wakiwa na alama 23.