Pedri azu gumzo kisa ujumbe wa siri uliotimia baada ya siku 400.
Joyce Shedrack
July 15, 2026
Share :
Kiungo wa Hispania Pedri amezua gumzo kubwa baada ya mashabiki kugundua ujumbe wa siri aliouchapisha takribani miezi 13 iliyopita.
Mnamo Juni 10, 2025, Pedri aliweka picha kwenye ukurasa wake wa kijamii na kuandika namba sita tu kwenye maelezo ya chapisho lake
19 07 26

Mashabiki wengi hawakuelewa maana ya namba hizo wakati huo baada ya kupita siku 400, imebainika kuwa tarehe hiyo ni 19 Julai 2026 siku ambayo imepangwa kuchezwa fainali ya Kombe la Dunia jijini New York, Marekani.
Chapisho hilo limevutia zaidi baada ya usiku wa jana Hispania kufanikiwa kufuzu kucheza fainali hiyo, jambo ambalo limewafanya wengi kuamini kuwa huenda Pedri alikuwa na ndoto au imani kubwa kuhusu safari ya timu yake.





