Penzi la Kizz Daniel lapumulia mashine.
Joyce Shedrack
July 17, 2024
Share :
Penzi la msanii wa Muziki kutoka Nigeria Kizz Daniel linatajwa kuwa matatani kuvunjika kutokana na ujumbe aliokuwa ameuchapisha msanii huyo kwenye mtandao wa X na badae kabla ya kuufuta.
Msanii huyo alichapisha ujumbe unaosomeka “Kama unataka kuvunja mahusiano na mimi hakuna shida wewe nilipe bili zangu kwa kila kitu nilichokufanyia muda wangu, zawadi zangu na vitu vingine vyote ndipo utaweza kuondoka”.
Baada ya kuchapisha ujumbe huo muda mfupi baadae aliufuta ujumbe huo ambao umefanya watu wengi kuhisi kwamba pengine aliuuchapisha kwa ajuili ya mke wake ambae wanatajwa kutokuwa kwenye maelewano muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinasema msanii huyo amepoteza uaminifu kwenye ndoa yake jambo lililopelekea mke wake MJay Anidugbe kukosa uvumilivu na kushindwa kumsamehe akitaka kuachana na msanii huyo.