Penzi la Mariah Carey na Tanaka lavunjika baada ya miaka 7
Eric Buyanza
December 21, 2023
Share :
Mwanamuziki mkongwe, Mariah Carey amerudi sokoni, amerudi sokoni kwa maana ya kwamba kwasasa yuko 'single' baada ya yeye na aliyekuwa mpenzi wake Bryan Tanaka kutangaza rasmi kuachana baada ya kudumu penzini kwa miaka 7.
Taarifa zinasema kuachana kwao kumekuja baada ya Bryan kutaka familia yaani (watoto) huku Mariah Carey akiwa hana mpango huo, kwani tayari ana watoto mapacha aliyezaa na mume wake wa zamani Nick Cannon.
Bryan mwenye miaka 40 anapishana miaka 14 na Mariah Carey ambaye kwasasa Mariah ana miaka 54