Penzi la Teyana Taylor na Aaron Pierre lavunjika.
Joyce Shedrack
December 31, 2025
Share :
Msanii wa Marekani Teyana Taylor na muigizaji Aaron Pierre wameripotiwa kuachana. Wawili hao walikuwa kwenye uhusiano mwaka 2024, na walionekana pamoja mara kadhaa kwenye matukio ya burudani na hadharani.
:max_bytes(150000):strip_icc():focal(960x303:962x305)/aaron-pierre-tayana-taylor-relationship-main-061225-1135e3fa47ed4fb1875faae6be75417a.jpg)
Hata hivyo, taarifa za hivi karibuni zinaeleza kuwa hawako pamoja tena. Sababu za kuachana kwao hazijawekwa wazi, na wote wawili hawajatoa tamko rasmi. Kwa sasa, kila mmoja anaendelea na maisha yake kivyake.
Wawili hao waliingia penzini ikiwa tayari teyana ametalikiana na mpenzi wake wa zamani ambaye alizaa naye watoto wawili walivyokua pamoja.





