pmbet

Pep amvulia kofia Benardo Silva

Sisti Herman

November 10, 2025
Share :

 

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amemvulia kofia kiungo wake Benardo Silva kwa jinsi alivyochezesha timu na kuisaidia kuibuka na ushindi wa mabasi 3-0 dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Etihad, ukiwa ni michezo wa ligi Kuu nchini England.

Uzuri wa Bernardo ulikuwa kuweza kupokea mpira katika maeneo ya kiungo yenye msongamano na kuchagua pakupeleka mpira kwa ufanisi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Licha ya nafasi yake ya kiungo cha chini kwa City, bado alikuwa mchezaji aliyecheza pasi zenye mafanikio zaidi katika tatu ya mwisho.

"Kwa jinsi tulivyocheza leo, yeye ni Masta" alisema Guardiola. "mijongeo, kuwania mpira, kuongeza kasi, kupunguza kasi, angalizo [kujua] nafasi iko wapi, jinsi ya kudhibiti hali na mambo mengi. Yeye ni mmoja wa wachezaji wajanja zaidi ambao nimewahi kukutana nao."

Bernardo alitabiriwa kuwa ufalme wake unakaribia mwisho hasa msimu uliopita, lakini Guardiola anakiri kwamba kushuka kwa kiwango cha uchezaji, ana mtazamo tofauti juu yake. "Bernardo alijitahidi msimu uliopita, lakini alikuwepo. Kila Mchezo. Amechoka. 

Baada ya dakika 50 au 60 [za mechi za msimu uliopita], hakuweza kukimbia dakika moja zaidi. "Wakati fulani, alisema, 'Pep, nimeishiwa nguvu. Akili yangu haipo [hapo] tena, miguu.' Lakini alikuwepo na nilisema mara nyingi kwa wachezaji wangu, na kwake, hilo halitasahaulika kwa sababu alikuwa nahodha wangu katika nyakati mbaya.

Kwenye michezo wa jana Bernardo alipiga pasi 19 kwenye eneo la tatu ya mwisho (final third), akifuatia na kiungo wa Liverpool Dominiki Szoboszlai aliyepiga pasi 16 kwenda eneo hilo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet